Songtexte.com Drucklogo

Nitayainua Macho Songtext
von Christina Shusho

Nitayainua Macho Songtext

Nitayainua macho yangu juu nitazame milima
Msaada wangu utatoka wapi?
Msaada wangu u katika Bwana
Majeshi yajapojipanga kupigana nami
Moyo wangu hautaogopa
Maana najua husinzi wala hutalala Bwana wangu utanipigania 2


Eeh Bwana nimeungojea wokovu wako na maagizo yako nimeyatenda
Nafsi yangu imezishika shuhuda zako nami nimekupenda mno
Nimeyashika mausia yako maana njia zangu zi mbele zako

Bwana kilio changu yakikukaribia unifahamishe sawa na neno lako
Dua yangu na ifike mbele zako uniponye sawa na ahadi zako
Midomo yangu na itoe sifa kwako ulimi wangu uimbe ahadi zako
Nafsi yangu na iishi ipate kukusifu hukumu zako zinisaidie 2
Eeh bwana... 2

Songtext kommentieren

Log dich ein um einen Eintrag zu schreiben.
Schreibe den ersten Kommentar!

Beliebte Songtexte
von Christina Shusho

Quiz
Wer ist gemeint mit „The King of Pop“?

Fans

»Nitayainua Macho« gefällt bisher niemandem.